Thursday, September 21, 2017

Everton yamkata Rooney mshahara wa wiki mbili


Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemlima adhabu ya kukatwa mishahara ya wiki mbili mshambuliaji wake Wayne Rooney kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalum.

Everton ina mradi wa kusaidia watu wasiojiweza na imesema fedha hizo zitasaidia sana.
Rooney mwenye miaka 31 aliomba kusahemewa ili aepuke adhabu hiyo.

Siku ya Jumatatu alikuhumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari huku amelewa, Atafanya pia kazi za jamii kwa siku mia moja.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo