Shirika la kimataifa la WaterAid
Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Uingereza- DFID linategemea
kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika za Lemanyata, Oltrumet na Olkokola halmashauri ya
Arusha.
Katika kata hizo mradi huo
unaokadiriwa kutumia zaidi ya shilingo bilionni 4 fedha za kitanzania unategemea
kuwanufaisha wananchi wa vijiji vya Olkokola na Lengijave pamoja na Vitongoji
vya Seuri, Ekenywa na Ngaramtoni.
Katika hatua za awali za utekelezaji
wa mradi huo, Mkurugenzi wa Shirika la WaterAid Tanzania Dk. Ibrahim Kabole
ameongoza timu ya wataalam wa maji kutembelea eneo utakapotekelezwa mradi huo
pamoja na kuzungumza na viongozi wawakilishi wa wananchi katika kata hizo mbili
na hatimaye kufanya mazungumzo na uongozi wa halmashauri.
Dk. Kabole ameelezea kuwa mradi huo
utakuwa ni mradi wa tofauti na miradi mingine iliyowahi kufanyika kwa kuwa utatumia
teknojia ya kisasa ya kuwahudumia wateja wa maji kwa kuwasajili kwenye kwenye
mfumo wa kielekroniki ambao utawawezesha kulipia maji kabla ya kutumia yaani ‘pre-paid’ mfumo ambao utasimamiwa na shirika la e-water.
Utofauti mwingi ni kuwa, mradi huu
wa maji unategemea kuwa ni mradi endelevu na shirikishi kwa wananachi wenyewe
watakaonufaika na zaidi utakaojumuisha wataalamu wa fani mbalimbali
kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Aidha Dk. Kabole ameuomba uongozi wa
halamshauri ya Arusha kutoa ushirikiano wa karibu wakati wa utekelezaji wa
mradi huo ili uweze kufanyika na kumalizika kwa wakati kwa kuwa wananchi wa
eneo hilo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama
kutokana na eneo hilo kuwa kame na maji kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya
Floraidi.
“Tunakwenda kuanza ujenzi wa maradi
wa maji, ili uende kwa haraka na kumalizika kwa wakati ninawaomba viongozi wote
wa serikali na siasa katika halmashauri kuwaeleimisha wananchi kuwa mradi huu
ni wao na hivyo wanantakiwa kutoa ushirikiano kwa wataalamu wote watakao husika
katika utekelezaji wa mradi jhuu” amesisitiza Mkurugenzi huyo.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa
Arusha Mhandisi Joseph Makaidi
amelishukuru shirika la WaterAid na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano kila mmoja kwa umuhimu wake na
kuwapongeza kwa kuwa wanatekeleza sera ya serikali ambayo inalenga ifikapo
mwaka 2020 asilimia 85% ya wananchi waishio vijijini kupata maji safi na
salama.
“Shirika linatekeleza mpango wa
serikali hivyo sisi kama serikali hatuna budi kuwapa support inayohitajika na
kuhakikisha mazingiora salama wakati wote wa uteklelezaji wa mradi mpaka
kukamilika kwake” alisema Mhandisi Makaidi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa halmashauri
ya Arusha Mhe. Noah Lembris ameahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa shirika
hilo na wadau wote wakati wote wa utekelezaji wa mradi huo ili uweze kumalizika
kwa wakati kwa faida ya wananchi wa maeneo hayo ambao wanakabiliwa na changamoto
kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama.
No comments:
Write comments