Madiwani halmashauri ya Arusha Mheshimiwa Yasimin Bachu Viti Maalum ( CCM) na Mheshimiwa Baraka Simon wakinadi sera zao wakati wa kuomba kuchaguliwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, uchaguzi unaoendelea kwenye Ukumbi wa zmikutano halmashauro ya Arusha.
Akiwasilisha taarifa ya muongozo na kanuni za Uchaguzi wa Makamu Mwenyeikiti wa halmashauri Mwanasheria wa halmashauri ya Arusha wakili Dustan Shimbo amefafanua kuwa uchaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa Sheria za serikali za mitaa sura ya 287 marejeo ya mwaka 2002 na Kanuni za Kudumu za zhalmashauri ya Arusha zMakamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Kamati za Kudumu wanapaswa kuchaguliwa baada ya mwaka mmoja ambao uliishia Januari 2017.
Uchaguzi unaendelea katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
No comments:
Write comments