Sunday, August 27, 2017

Sitarajii kupigana tena: Mayweather


Bondia Floyd Mayweather amesema kwamba hatapigana tena na kuthibitisha kuwa hatarajii kuonekana tena katika ulingo wa ndondi baada ya kumshinda Conor McGregor katika pigano lililomalizika kwa njia ya knockout katika raundi ya 10.

Licha ya uamuzi huo bondia huyo amesema kuwa atapanda ulingoni kwa sharti kubwa kwamba endapo atapata fursa ya kujipatia dola 300m kwa dakika 36 atarudi.

''Mimi sio mjinga, iwapo kutakuwa na fursa ya kutengeza dola $ 300m katika dakika 36 nitarudi kupigana''.

Mayweather ambaye alistaafu baada ya kumshinda Andre Berto mnamo mwezi Septemba 2015 amesema kuwa hakuna kilichosalia kudhihirishia ulimwengu.

Mayweather ameongeza kuwa hili ni pigano langu la mwisho hamutaniona tena.Mtu yeyote anayetaka kupigana nami asahau, ninajiandaa kuwa mkufunzi wa ndondi ili kuwasaidia mabondia.

Mayweather alikiri kwamba pigano dhidi ya McGregor lilimchukua muda mrefu kumsimamisha mpinzani wake zaidi ya walivyodhania yeye na babake.

''Nilifanya kile ninachoweza kufanya'', alisema. ''Nilipata njia ya kumnasa na kufanikiwa kumpiga.Babangu alidhani kwamba nitamsimamisha katika raundi ya saba ama hata sita''.
''ilituchukua muda mrefu lakini hatimaye tulifanikiwa kufanya kile tunachoweza kufanya''.

Wakati wa pigano hilo Mayweather alionekana kukasirishwa na hatua ya McGregor kumpiga kisogoni.

''Nilimwachia refa kufanya kazi yake,alisema.Siko hapa kumshutumu refa lakini muliona kilichokuwa kikiendelea''.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...