Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo kwa kuthibitisha kuwa matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais huyo alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa.
Rais Kagame amefanikiwa kutetea kiti nafasi hiyo ya urais ambayo amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa na kwa ushindi huu atahudumu nafasi hiyo muhula wa tatu wa miaka saba.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa, Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana.
Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.
No comments:
Write comments