Na. Elinipa Lupembe.
Shirika lisilo la kiserikali la Tumaini Jipya lenye makazi yake kata ya Olkokola halmashauri ya Arusha limeonesha kuridhishwa na utekelezaji wa shughuli za kuwahudumia wananchi zinazofanya na halmashauri hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza kwa njia ya mtandao mkurugenzi na mwanzilishi wa shirika hilo Bi. Louise Richardson raia wa Uingereza amesema kuwa ameridhishwa na utekeleza shughuli za kuwahudumia wananchi katika halmshauri ya Arusha kwa ili kutatua changamoto za huduma za kijamii zinazowakabili wananchi hasa wa maeneo ya vijijini.
Louise ameoneshwa kuridhishwa zaidi na utekelezaji wa mradi wa maji wa vijiji vitano mradi ambo yeye binafsi ndiye chanzo cha upatikani wa ufadhili wa mradi huo kutoka nchini kwake Uingereza, baada ya kushuhudia adha ya maji wanaipata hasa watoto wakike wawapo shuleni na kuamua kurudi nchini kwao kutafuta fedha za kutekeleza mradi wa maji.
Hata hivyo Louise amesema hayo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mkuu wa Kitengo cha huduma ya Jamii 'DFID' Bi. Getrude Mapunda aliyetembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo wa maji mwishoni mwa wiki iliyopita, ameanza kuona upatikanaji wa huduma ya maji katika vijiji hivyo ambavyo kiuhalisia wana shida kubwa ya upatikani wa maji safi na salama.
Amesisistiza kuwa lengo hasa la shirika la Tumaini Jipya ni kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kuhakikisha huduma zote za jamii zinawafikia wananchi hasa waishio vijijini na kufafanua kuwa endapo mradi huo utatekelezwa kwa wakati na kwa viwango na jamii kushiriki katika utunzaji na uchangiaji wa huduma za maji ili huduma hizo ziwe endelevu, serikali ya Uingereza itaendelea kutoa misaada mingi kupitia shirika lake la Tumaini Jipya.
Shirika la Tumaini Jipya limekuwa likifadhili shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo uwekaji vioo kwenye vyumba vya madarasa shule ya msingi Olbaki pamoja na kweka miundombinu ya umeme kwenye nyumba za walimu wa shule hiyo pamoja na zahanati ya kijiji cha Lengijave .
Licha ya misaada hiyo Louise ametoa msaada wa mashine ya kusaga nafaka ili kutatua changamoto inayowakabili wakazi wa kijiji cha Lengijave ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo, mradi huo utakaoanza kufanya kazi mara baada ya mchakato wa kuingiza umeme kukamilika.
Hata hivyo Louse amesema kuwa shirika la Tumaini Jiya liko tayari kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwenye sekta za elimu, afya na maji nchini Tanzania kutokana na mapenzi mema aliyonayo hasa kwa wananchi wa kijiji cha Lengijave eneo ambalo amewahi kuishi kama 'volontia'.
Bi. Louise ambaye ni Diwani nchini Uingereza, ndiye chimbuko hasa la mradi wa maji wa vijiji vitano baada ya kukerwa na changamoto ya ukosefu wa maji hasa kwa watoto wakike wawapo shuleni na kuamua kurudi nchini kwao kutafuta fedha, Mradi wa maji wa vijiji vitano unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia wa na Idara ya Maendeleo ya kimataifa 'DFID' na kutekelezwa na shirika la WaterAid- Tanzania.
No comments:
Write comments