Katika Mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu kati ya Yanga na Lipuli FC katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam huku mabingwa wa tetezi wa ligi kuu Tanzania bara wakilazimisha sare ya goli 1-1 katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi walionekana kushindwa kuonyesha mbwembwe zao dhidi ya Lipuli huku Tshishimbi akiwemo katika kikosi hicho.
Timu ya Lipuli ya mjini Iringa ndio kwanza wamerudi katika ligi kuu baada ya kupotea kwa kushuka daraja miaka kadhaa iliyopita na kuanza ligi ya sare na mabingwa watetezi wa ligi hiyo.
Katika mchezo huo kinara wa Lipuli Seif Abdallah aliing'arisha timu yake kwa kuipatia Goli la kwanza dakika 44 kabla ya Donald Ngoma hajasawazisha goli hilo dakika ya 46 lilodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Akizungumza baada ya mchezo huo Seif Abdallah amesema "Nina furaha sana kufunga goli langu la kwanza baada ya kurudi kwenye ligi kuu. Huu ni muendelezo wa rekodi yangu kila ninapokutana na Yanga"
Pamoja na hayo Lipuli wamepata doa baada ya kucheza pungufu dakika za majeruhi baada ya Nahodha wa timu hiyo Asante Kwasi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na maamuzi yaliyotolewa na refa wa mchezo.
Kuhusu msimamo wa raundi ya kwanza Simba SC wanaongoza kwa magoli 7 na pointi 3 nafasi ya 1 huku watani zao yanga wakiwa nafasi ya 9, pointi 1 na goli 1.
No comments:
Write comments