Thursday, August 10, 2017

Ajali ya ndege yaua Arusha

Mtu mmoja rubani wa ndege amefariki dunia baada ya ndege aliyokuwa akiingoza kuanguka na kusababisha kifo chake wakati ikitokea uwanja wa ndege Arusha ikielekea Serengeti mkoa wa Mara. Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Safari Air Link ambayo ilikuwa ikitokea Arusha kuelekea Serengeti mkoani Mara kwa ajili ya kuchukua abiria, ilianguka na kusababisha kifo cha rubani huyo. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo amesema kuwa ndege hiyo aina ya Cessina 206 yenye namba za usajili 5H-SAL 206 ilianza safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Arusha jana muda wa saa 1:05 Asubuhi ikiwa na rubani pekee na muda wa saa 4:00 Asubuhi taarifa za kuanguka ndege hiyo zilianza kusikika. Kamishna Mkumbo amefafanua kuwa mara baada ya taarifa ya kuanguka ndege hiyo muda wa saa 6:30 Mchana, ndege hiyo ilionekana na kubainika kuwepo kwa mwili wa mtu mmoja ambaye ni Rubani aliyejulikana kwa jina la David Mbale (25) mkazi wa jijini Dar es saalam. Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria watano ilianguka jana katika milima ya Monduli kijiji cha Engalaon kilichopo wilaya ya Arumeru mpakani na wilaya ya Monduli huku chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na kuaelezea kuwa uchunguzi wa tukio hilo unafanywa na wataalamu ili kubaini chanzo cha ajali hiyo . Mwili wa Marehemu David Mbale umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...