Na. Elinipa Lupembe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo ameagiza kujengwa jengo jipya la upasuaji katika kituo cha Afya Nduruma na chumba cha upasuaji kilichopo na badala yake jengo hilo kutumika kwa kazi nyingine kutokana na jengo hilo kuonekana kuonekana kuwa dogo kulingana na matarajio ya huduma inayotegemewa kutolewa katika kituo hicho.
Waziri Jafo amesema hayo wakati wa kuweka Jiwe la Msingi katika kituo cha hicho cha Afya halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua ujenzi na upanuzi wa miundo mbinu unaoendelea kituoni hapo.
Licha ya Waziri Jafo kushauri kuanza ujenzi wa jengo jipya la upasuaji na kuacha la zamani lakini pia amekiri kuridhishwa na ujenzi huo wa miundo mbinu yote unaoendelea na kuongeza kuwa huo ni utekelezaji wa agenda kuu ya serikali ya awamu tano ya kuboresha sekta ya Afya.
Ameongoza kuwa katika kutekeleza hilo, katika mwaka wa fedha uliopita serikali ilitenga bajeti ya shilingi milioni 172 kutoka bilioni 31 za awamu ya nne na kufanikiwa kuboresha jumla ya vituo vya afya 172 nchi nzima na vituo 205 vipo kwenye mpango.
Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt. Wilson Mahera amesema kuwa kituo hicho kilianza kama zahanati mwaka1951 na mwak 2014 kilipandishwa hadhi ya kuwa kituo cha afya.
Dkt. Mahera amesema kuwa kituo hicho cha afya kinalabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi 28 kulingana na muongozo wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ya mwaka 2014 hadi 2019 na kwa sas kituo kina watumishi 11 tuu.
Katika hali ya unyenyekevu wa hali ya juu Mbunge wa viti maalumu anayewakilisha Mkoa wa Arusha Mhe. Amina Mollel amesema Wananchi wa Nduruma wanaishkuru Serikali kwa kuwaboreshea kituo cha Afya Nduruma na wanaomba zaidi msaada wa kupata Gari la kubebea wagonjwa ili iwe rahisi kuwatoa katika kituo hicho na kuwapeleka katika Hospital ya rufaa pindiitakapotokea dharura ya kufanya hivyo.
" Mhe Waziri sisi wananchi wa Nduruma tunakushkuru sana kwa namna ambavyo Serikali inatuboreshea huduma za Afya lakini bado shida zetu hazijaisha, tunaomba mtusaidie Gari la kubebea wagonga na matengenezo ya barabara yetu tutashukuru zaidi" Alisema Mhe. Mollel.
Hata hivyo Waziri Jafo ameahidi kuyashughulia maombi yote yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mollel na kwa kuanzia amemuagiza Maneja wa TARURA halmashauri ya Arudha kuanza ukarabati mdogo wa barabara hiyo huku wakiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa na wa kudumu na kuahidi kushugulikia mahitaji mengine yote kadiri fedha zitakavyopatikana.
Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa miundo mbinu ya kituo hicho cha Afya na baada ya ujenzi huo kukamilika Kituo kitakua na wodi ya mama na mtoto, Maabara, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia maiti, kichomea taka, sehemu ya kufulia nguo pamoja na nyumba ya daktari na kufanya kituo hicho kuwa na hadhi ya nyota tano.
PICHA ZA MATUKIO YA SHUGHULI HIYO.
No comments:
Write comments