Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan amezindua huduma mpya ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL- pesa ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL.katia hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais amesema kuwa uzinduzi wa huduma ya TTCLpesa ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo kurejea katika nafasi yake ya awali ya kuwa suluhisho la kweli la utoaji huduma za Mawasiliano hapa nchini.
“Huduma hii ni uthibitisho mwingine kwamba TTCL inatekeleza kikamilifu maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuyataka Mashirika yote ya Umma kujiendesha kwa faida na kutoa gawio Serikalini pamoja na kuwahudumia wananchi kwa kiwango cha juu na cha ubora na kwa gharama nafuu” Makamu wa Rais.
Aidha, Makamu wa Rais amethibitisha huduma zitakazopatikana kwa kutumia TTCpesa ni pamoja na kutuma na kutoa pesa kwa viwango vya chini kabisa kupita mitandao yote, kulipia LUKU,ankara za Maji, Ving’amuzi, kununua muda wa maongezi na vifurushi vya data vya TTCL.
Hata hivyo Makamu wa Rais amesema kuwa serikali imejipanga kukabiliana na kutatua changamoto zinazolikabili shirika la TTCL na kuwataka watumishi wa shirika hilo kutumia vyema rasilimali walizopewa ikiwemo Mkongo wa Taifa na Kituo cha Kuhifadhia Kumbukumbu za kimtandao kupata pesa za kujiendeshea.
Makamu wa Rais pia aliipongeza menejimenti ya TTCL kwa wazo lao la kufikiria kuanzisha kiwanda cha simu hapa nchini. Alisema “msisitizo wa serikali yetu kwa sasa ni ujenzi wa uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025 kupitia uwekezaji katika viwanda hivyo wazo lenu la ujenzi wa kiwanda cha simu limekuja wakati muafaka”.
Katika hfla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir i Kindamba alipata fursa ya kumuonesha Makamu wa Rais mama Samia Suluhu namna ya kutumia huduma ya TTCLpesa mara baada ya uzinduzi huduma hiyo.
No comments:
Write comments