Arusha.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amehoji uhalali wa nyumba za ibada kujengwa ndaniya Uwanja wa maonyesho Nanenane eneo la Njiro mkoani Arusha. Mkuu wa mkoa huyo ameshangazwa pia kuona ndani ya mabanda hayo kuna watu wanaishi na kusema ipo sababu ya kuhoji uhalali wa watu hao kuishi ndani ya viwanja hivyo pamoja na makanisa yakiwa ndani ya eneo la mabanda ya maonyesho hayo. Hata hivyo Gambo amelazimika kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuchunguza ubadhirifu wa mali na fedha uliofanyika kwenye mabanda hayo maonesho ya Nanenane. Amesema maandalizi ya maonyesho ya nanenane yataandaliwa na ofisi yake kupitia kwa katibu tawala na si Chama cha Wakulima na Wafugaji Tanzania,(TASO) kama ilivyozoeleka. "Sababu za kukatazwa kushiriki maonyesho hayo kwa nchi nzima ni kutokana na utendaji kazi wao mbovu na ubadhilifu wa fedha, hivyo tunatekeleza agizo la serikali " Mpaka sasa maandalizi ya maonyesho ya Nanenane yanaendelea vizuri na tunategemea Makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu anategemewa kuzindua maonesho haya,"amesema Gambo Mkuu wa mkoa wa Manyara John Bendera ,amesema maagizo ya kutoshiriki kwenye maandalizi ya maonyesho kwa TASO ni maagizo ya kiserikali kutokana na chama hicho kushindwa kutenda kazi zao. Amesema pamoja na agizo hilo,bado wako kwenye mikakati ya kukabidhiana majukumu na chama hicho na kuwataka wananchi wanaotaka kushiriki maonyesho hayo kwenda kulipia mabanda yao kwa katibu tawala wa mkoa Arusha na si TASO kama ilivyokuwa hapo awali.
Sunday, July 23, 2017
RC Gambo ahoji uhalali wa nyumba za ibada uwanja wa nanenane Arusha

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments