Monday, July 17, 2017

Halmashauri ya Arusha yakusanya mapato kwa asilimia 92.01% mwaka wa fedha 2016/2017




Madiwa wa halamshauri ya Arusha kwa pamoja watoa pongezi kwa uongozi wa halmshauri hiyo kwa kukusanya mapato kwa asilimia 92.01% kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2016/2017.

Pongezi hizo zimetolewa kwenye Mkutano wa Baraza la madiwani wa robo ya nne ambayo ni mkutano wa mwiasho kwa mwaka wa fedha 2016/17 baada ya Mhasibu wa Mapato ndugu Shabani Kisija  kuwasilisha taarifa ya mapato na matumiza kwa mwezi Juni 2017 kwa niaba ya Mweka hazina wa halmashauri.

Kisija aliwasilisha taarifa hiyo kwa kuwaeleza wajumbe wa baraza la madiwani kuwa hadi kufika Juni 30 2017 halmashauri imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.9 sawa na asilimia 92.01% kutokana na makisio ya shilingi bilioni 3.2.

Hata hivyio Kisija amefafanua kuwa kutokana na mapato hayo halmashauri imetumia kiasi cha shilingi bilioni 2.9  kwa maeneo yasiyo ya ruzuku sawa na asilimia 991.55%  na pia imetumia kiasi cha shilingi milioni 36.1 kwa maeneo yasiyo ya ruzuku na mishahara sawa na asilimia 96.80%.

Naadhi ya wajumbe waliop[ongeza makusanyo hayo ni pamoja na mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi mheshimiwa Gibson Ole Meseyeki kwa kusema kuwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 92% ni jambo la kujivunia na niwakati mzuri wa kuandaa mikakati thabiti ya kukusanya zaidi kwa mwaka unaoanza.

" Mheshimiwa mwenyekiti nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi wa halmshauri kupitia baraza lako pamoja na wataalamu, Idara ya fedha wakiongozwa na mkurugenzi kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kuwa haijawahi kutokea, ila niombe tupange mikakati thabiti ya kukusanya zaidi kwa mwaka huu tufike asilimia mia moja na zaidi" amesisistiza Mbunge Meseyeki.

Diwani wa kata ya Mwandeti Mheshimiwa Bonifasi Tarakwa amesifu pia juhudi za halamshauri kwa kukusanya mapato kufikia asilimia 92% licha ya changamoto nyingi zilizojitokeza katika ukusanyaji wa mapato na vyanzo vya mapao.

Mwenyekiti wa halmshauri ya Arusha mheshimiwa Noah Lembris amehitimisha mkutano huo kwa kutoa pongezi kwa mkurugezi na timu ya wataala , Kamati ya fedha na wananchi wa halmashauri ya arusha kwa kuitikia mwito wa kulipa kodi nakuwataka wataalamu kuendelea kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi na kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo