Baraza la Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni, halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru limepata mjumbe mpya baada ya kuapishwa kwa Mheshimiwa Penina Mollel wakati wa Mkutano wa robo la robo ya pili la Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Zoezi la kuapishwa kwa mheshimiwa Penina limefanywa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Usalama Wakili Dustan Shimbo mbele ya wajumbe wa Baraza hilo na kushuhudiwa na watu wote waliokuwepo ukumbini hapo.
Wakili Shimbo amesema kuwa kuanzia sasa Mheshimia Penina Mollel ni mjumbe halali wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni na anaruhusiwa kufanya shughuli zote za baraza hilo kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo Wakili Shimbo ametumia muda huo kutolea ufafanuzi sheria, taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali ya utoaji na uchangia wa hoja wakati wa baraza pamoja na kufuata kanuni za utoaji maazimio hasa yale yanayohitaji maamuzi ya ngazi za juu kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Akizungumza baada ya kuapishwa mheshimiwa Penina amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na wajumbe wa Baraza hilo na kuwa mtii kwa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na kutekeleza Ilani ya Chama chake cha CCM pamoja na kuwatumikia wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni.
Mheshimiwa Penina ameteuliwa kuwa mjumbe wa viti Maalum wa Serikali ya kitongoji kupitia Chama cha Mapinduzi CCM na kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Mary Merisori aliyefariki dunia mwaka 2017.
Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni linaundwa na Wenyeviti wa Vitongoji 21 vilivyo ndani ya kata saba za Moivo, Ilboru, Kiranyi, Oloirieni, Tarakwa, Ngaramtoni na Olturumet.
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUAPISHWA MH. PENINA MOLLEL
No comments:
Write comments