Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Noah Lembris amewataka wataalam wa ngazi za vijiji na kata kutumia muda zaidi kujifunza matumizi ya 'Force Akaunti' katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao.
Mheshimiwa Noah amesema hayo alipoongoza jopo la Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekeleza katika mwaka wa fedha 2017/2018, ziara inayofanyika kila robo ya mwaka wa fedha.
Mwenyekiti huyo amesisitiza hayo baada ya kugundua kuwa bado kuna baadhi ya viongozi wa vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto ya namna ya kufuata utaratibu halisi wa matumizi ya fedha za miradi zinazopelekwa katika maeneo yao na kuwa na mkanganyiko wa nini hasa kifanyike kutekeza miradi hiyo kwa kutumia forced akaunti.
" Kuna maeneo machache ambayo watalamu wa ngazi za vijiji na kata bado wanakabiliwa na changamoto ya namna ya kutumia force akaunti katika kutekeleza miradi ya maendeleo hasa katika matumizi ya local fundi na mkandarasi ni vyema kujifunza hilo ili kuondoa mkanganyiko huo" amesema Mwenyekiti huyo
Aidha Mwenyekiti Noah amewataka wataalamu wa halmashauri katika Ofisi ya Mipango na Idara yenye mradi kufanyakazi kwa karibu na maafisa watendaji wa kata na vijiji na uongozi wa vijiji pindi wanapopeleka fedha za miradi ili kuhakikisha taratibu za matumizi ya force akaunti zinafuatwa.
Licha ya changamoto hiyo iliyojitokeza kwenye miradi michache Wajumbe wa Kamati hiyo wameonedha kuridhishwa na utekelezaji wa miradi mingi uliotumia force akaunti na kufuata taratibu zote ambayo imeonesha mafanikio makubwa tofauti na hapo awali serikali ilipokuwa inatumia wakandarasi kwenye miradi.
Licha ya changamoto hiyo Wajumbe hao wameridhishwa kwa asilimia kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo waliyoikagua na kuthibitisha ulinganifu wa thamani ya fedha na ubora wa miradi hiyo 'value for money' inayoonekana hata kwa macho.
Wameongeza kuwa matumizi ya 'force akaunti' yanaonesha mafanikio makubwa hasa katika ushiriki wa wananchi wa maeneo husika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo jambo ambalo linaongeza umiliki wa miradi hiyo kwa wananchi na kuona kuwa miradi hiyo ni mali yao.
Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati ya Fedha wamefanikiwa kutembelea na kukagua jumla ya miradi 20 yenye thamani ya shilingi milioni 822.4 katika sekta za elimu, afya, maji na Maendeleo ya Jamii liyoko kwenye kata za Nduruma, Bwawani, Oljoro, Laroi, Musa, Mwandeti,Olturumet, Kimnyaki, Sambasha,Kiranyi na Ilkiding'a.
PICHA ZA MATUKIO YA ZIARA HIYO.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya Sayansi shule ya Sekondari Olemedeye kata ya Nduruma. |
Jengo la kuhifadhia maiti linalojengwa kwenye kituo cha Afya Nduruma |
Add caption |
No comments:
Write comments