Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ameandika barua ya kujiuzuru nafasi yake mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwataka wateule wake wote waliotajwa kwenye ripoti ya biashara ya madini ya Almasi na Tanzanite kujiondoa wenyewe ili kupisha vyombo vya usalama kufanya kazi yao.
Akiongea mara baada ya makabidhiano ya ripoti hizo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na sasa anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.
“Hata sasa unanichelewesha nipo naandika barua ya kujiuzulu, hii ni nafasi niliyopewa na ni lazima nimuunge mkono Rais katika hatua zake za kutaka kubadili mfumo wa nchi na kuufanya wenye manufaa kwa wananchi,” amesema Ngonyani.
Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.
No comments:
Write comments