Thursday, September 7, 2017

Waziri Simbachawene ajiuzuru


Muda mfupi baada ya agizo la mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwataka wateule wake waliotajwa kwenye ripoti ya madini ya Almasi na Tanzanite  kujiondoa wenyewe Waziri Simbachawene amejiuzuru nafasi yake ya uwaziri.

Simbachawene amewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na madini Mei 2012-Janauri 2014, baada ya hapo akahamishiwa kwenye Wizara ya Nyumba na Makazi katika nafasi ya Unaibu waziri, na ilipofika Januari 2015 akateuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini akichukua nafasi ya Prof Sospiter Muhongo aliyejiuzulu kufuatia kashfa ya Sakala la Uchotwaji wa Fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo