BREAKING: Tundu Lissu Apigwa Risasi
MUUNGWANA BLOG / 15 hours ago
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mkoa wa Dodoma baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.
Dereva wake akiwa ameshika nguo na viatu vya Tundu Lissu
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.
Gari la Mbunge Lissu likionekana na baadhi ya matundu zilipopigwa Risasi
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba baada ya kuzinduka Lisu amesafirishwa na kupelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibsbu.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa amesema kuwa hali ya Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa.
No comments:
Write comments