Tuesday, August 8, 2017

Shughuli ya kuhesabu kura yaanza Kenya


Shughuli ya kuhesabu kura imeanza nchini Kenya muda mchache uliopita baada kumalizika zoezi la kupiga kura.

Baadhi ya vituo vilivyofunguliwa mapema na raia wengi walijitokeza kupiga kura na kufanya zoezi la upigaji kura kukamilika na sasa shughuli ya kuhesabu kuhesabu kura hizo imeanza.

Hata hivyo baadhi ya vituo vilivyofunguliwa kuchelewa vinaendelea kupiga kura huku tume ya IEBC ikisema kuwa vitangozewa muda kuendelea na zoezi hilo.

Raia wa Kenya walijitokeza kwa wingi mapema alfajiri milolongo mirefu ya kupiga kura ilishuhudiwa katika maeneo ya kupigia kura nchini humo ingawa vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi.

Wengi wa wapiga kura walipiga kambi katika vituo hivyo usiku kucha wakisubiri kutekeleza haki yao ya uchaguzi.

Baadhi ya vituo vilishuhudia mvua kubwa na hivyobasi kuathiri operesheni za shughuli hiyo .

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo