Tuesday, August 8, 2017

Mgombe Urais Kenya akwama kupiga kura


 Mgombea wa Urais nchini Kenya  Dr. Ekuru Aukot amekwama kupiga kura baada ya mafuriko kuvunja na kulisomba daraja la huko kaunti ya Nginyang kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta amepiga kura kwenye kituo cha shule ya Msingi Mutomo, Gatundu Kusini akiwa ameambatana na mkewe Margaret.

Naye Mgombea urais wa muungano wa Nasa Raila Odinga amepiga kura katika Kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Old Kibera.

Hata hivyo Mvua kubwa iiliyonyesha nchini humo imekwamisha zoezi la upigaji kura katika maeneo mbalimbali ikiwemo Turkana, Baringo na Samburu.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo