Mradi huo wa maji tayari umeanza kwa kufanya upembuzi yakinifu na unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
nchini Uingereza (DFID) utakao gharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 1.6 sawa na fedha za Tanzania
shilingi 426,607,17 kwenye kata za Lemanyata, Olkokola na Oltrumet
halmashuri ya Arusha.
Mkurugenzi wa Shirika la WaterAid Tanzania Dk. Ibrahimu
Kabole amesema lengo la semina hiyo elekezi ni kuutambulisha mradi huo kwa
wadau ili kuwa na uelewa wa pamoja kwa wahusika wote wataoshiriki katika
kutekeleza mradi pamoja na kufahamu gharama za mradi.
Dk. Kabole alizitaja taasisi zitakazo husika kutekeleza mradi huo ni pamoja na Halmashauri ya Arusha ambao ndiye mdau mkubwa wa mradi na kazi kubwa ya halamshauri ni kuratibu mradi huo kwa kupitia wataaalamu wake kwa kushirikiana na sekretarieti ya mkoa wa Arusha na kuhakikisha miongozo, taratibu na sera za maji, uchimaji wa maji na usafi wa mazingira.
Akifafanua shughuli za taasisi hizo Dk. Kabole ameeleza kuwa,
shirika la e-Water pay ambalo
kazi yake kubwa ni kfunga mfumo wa malipo wa kielektroniki unaojulikana kama e-WATER pay system kwenye vituo vya
kuchotea maji na kutoa kadi ‘tags’ kwa wateja pamoja na kufunga mfumo huo kwa
Mamlaka ya Maji Ngaramtoni (NGAUWASA) na vyombo vya watumia maji vijijini (COWSO).
Aidha Dk. Kabole ameelezea shughuli zitakazo fanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi cha Nelson Mandela ni pamoja na ukusanyaji wa takwimu za awali na kutengeneza viashiria na kuchangia upembuzi yakinifu ili kuwezesha utekelezaji wa mradi.
Mwenyekiti wa Halamshauri ya Arusha Mheshimiwa Noah Lembris amewataka viongozi wote wa kisiasa kuwaelimisha wananchi katika ameneo yao umuhimu wa kuchangia huduma ya maji ili huduma hiyo iwe enedelevu na kuachana na mawazo ya kuwa huduma ya maji ni bure.
"Viongozi tunawajibu mkubwa wa kuwaelimisha wananchi katika maeneo yetu kuondoa fikra za kuwa maji ni mali yetu hatutakiwi kulipia, dhana hiyo ni ya zamani isiyokuwa na tija kwa sasa, ili huduma ya maji iweze kuwa sustainable lazima watumiaji wachangie huduma hiyo, niwasihi viongozi wenzangu nendeni mkawaelimisha wananchi wenu kuwa mambo yanabadilika" amesisistiza Mwenyekiti huyo
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Dk. Wilson
Mahera ameshauri kuwa mtaalam atakayefanya upembuzi yakinifu ‘visibility study’ ahakikishe anafanya kazi kulingana na uhalisia wa eneo husika ili kuepusha hasara inayoweza kutokana na
mapungufu yanatokana na wataalamu hao.
“Tumepata tatizo kwenye miradi mingi iliyosababishwa na
Consultants wa visibility study kwaanda taarifa zenye mapungufu mengi, michoro isiyokuwa
na uhalisia jambo ambalo limesababisha hasara kwa ongezeko la gharama kwa
baadhi ya miradi na tatizo la miradi kukosa maji mara baada ya kukamilika”
amesisitiza Dk. Mahera
Wadau walioshrikishwa katika semina hiyo elekezi ni wataalamu
wa sekretarieti ya mkoo wa Arusha, wataalam wa halmashauri ya Arusha, viongozi wa serikali ngazi ya kata, Vijiji na Vitongoji, viongozi siasa ambao ni wawakilishi
wa wananchi, pamoja na viongozi wa Kamati za maji wa vijiji na vitongoji ambavyo mradi huo
unatekelezwa.
Picha za baadhi ya washiriki wa semina elekezi.
No comments:
Write comments