Thursday, July 6, 2017

TCRA Imetoa masharti 4 kwa mitandao simu kuanzia Julai 6



 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa masharti na vigezo ambavyo mtoa huduma za mawasiliano anatakiwa kuzingatia ikiwa ni siku chache tangu Mamlaka hiyo kutoa angalizo kwa watoa huduma baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa mawasiliano kukerwa na huduma za matangazo ya watoa huduma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo July 6, 2017 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema utaratibu huo ni kinyume cha matakwa ya Kanuni za Huduma za Ziada (VAS Regulations) za 2015 na Kanuni za Kumlinda Mtumiaji (Consumer Protection Regulations) za mwaka 2011.

Aidha, TCRA imesema kuwa, kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Ziada, baadhi ya masharti na vigezo ambavyo mtoa huduma (service provider) anatakiwa kuzingatia katika kutoa huduma ni pamoja na:-

1: Watoa huduma wanatakiwa kutoa taarifa kwa ukamilifu, (kwa Kiingereza na, au kwa Kiswahili), kuhusu huduma lengwa kwa kuendana na wakati na kwa lugha rahisi nay a kueleweka.

2: Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia matakwa ya Sheria na Kanuni za Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Mwaka 2001.

3: Watoa huduma wanaweza kutoa matangazo na taratibu za kujiunga na huduma mbalimbali za ziada wakati:

- wa kumjibu mteja anapouliza salio la muda wa maongezi;
-  mteja anapopokea taarifa baada ya kuongeza salio;
-mteja anapoingia kwenye orodha ya huduma za mtoa huduma.

4: Mtoa huduma haruhusiwi kutoa matangazo mengine yoyote kwa njia za mawasiliano ya simu au kwa njia yoyote ya kielektroniki bila kuzingatia vigezo vilivyowekwa kisheria.

Aidha TCRA imewataka watoa huduma wote kusitisha mara moja utoaji wa matangazo kwenye hduma za mawasiliano yasiyozingatia Kanuni za Huduma za Ziada (VAS Regulations) za mwaka 2015 kuanzia July 6, 2017.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo