Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Angela Mvaa amesema kuwa uzoefu unaonesha miradi mingi ya maji inashindwa kujiendesha kutokana na ukosefu wa fedha za kuendesha miradi hiyo.
Mvaa amefafanua kuwa mkakati wa serikali ni kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu kwa kujiendesha yenyewe ambapo wananchi wanatakiwa kuchangia huduma ya maji na kuwa na vyombo vya kisheria vya kusimamia miradi hiyo.
"Serikali inatengeneza miundo mbinu ya maji kwa gharama kubwa lakinj baada ya muda mfupi shida ya maji inarudi pale pale, kutokana na kuwa hakuna fungu la kukarabati endapo kutatokea uharibifu hata mdogo" amesema Mvaa
Naye Meneja wa maji Mamlaka ya Maji Ngaramtoni ndugu Clayson Kimaro ameongeza kuwa kutokana na changamoto ya usimamizi wa miradi ya maji Serikali imetunga Sera ya maji ya mwaka 2002 ambayo inataka kuundwa kwa vyombo vya watumia maji mijini na vijijini ambavyo vitasimamia uendeshaji wa miradi ya maji kwa wananchi kulipia huduma ya maji.
Kimaro ameendelea kueeleza kuwa faida za kuwa kwenye Mamlaka ya Maji ni kuwa mwananchi atahusika kulipia maji na kupata huduma na hatahusika na ukarabati wa miundombinu ya maji endapo kutatokea uharibifu.
Uzoefuinaonyesha watu wanaolipia maji wanamaendeleo kutokana na kuwa muda aliotakiwa kutumia kutafuta maji anatumia kufanya shughuli nyingine za kiuchumi" amesema Kimaro
Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji cha Lemanyata Thomas Meirura mesema kuwa wamefikia uamuzi wa kujiunga na mamlaka hiyo kwa lengo la wananchinkupata maji ya uhakika na mradi wa maji usimamiwe na chombo hicho kinachotambulika kisheria.
Ameongeza kuwa katika kijiji chao hakuna chombo cha kisheria cha kusimamia maji jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapo na kukubali kulipia huduma ya maji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maji ndugu Richard Mollel amethibitisha kutumia maji ambayo waliyakuta tangu enzi za mkoloni na miundo mbinu yake ni mibovu hivyo inasababisha uhabifu wa mara kwa mara na kuongeza kuwa hakuna mfuko maalumu kwa ajili za matengenezo.
"Inapotokea uharibifu wowote Kamati inalazimika kuchangisha fedha kwa ajili ya kutengeneza na wakati mwingine mtu hana pesa, tunakaa bila maji mpaka pesa ipatikane ya kutengeneza, uchangishaji unachukua muda mrefu "amesema Mollel.
Aidha wanakamati hao waliwachagua wajumbe wawili ambao watakuwa wajumbe wa Bodi ya NGAUWSA kuwakilisha kiji cha Lemanyata na fundi mmoja ambaye ataajiriwa na Mamlaka hiyo ya maji.
Akiwataja wajumbe waliochaguliwa ni ndugu Richard Meshilieki ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maji na ndugu Saning'o Meleki pamoja ndugu Zakayo Lootha amechaguliwa kuwa fundi.
Mradi wa maji wa WaterAid unatekelezwa kwenye vitongoji vya Ekenywa, Seuri na Ngaramtoni vyote vya Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni na viji viwili vya Lengijave na Lemanyata ambavyo vimekubali kujiunga na Mamlaka ya Maji Ngaramtoni ili mradi huo usimamiwe na mamlaka moja.
No comments:
Write comments