Tuesday, October 31, 2017

Madiwani watafuta muafaka wa Mita 200 zilizochukuliwa na Jiji la Arusha



Wajumbe wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wilayani Arumeru wametaka kukutanishwa na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Jiji la Arusha kuzungumzia namna ya kurudishiwa eneo la mita 200 kutoka barabara ya Moshi-Arusha-Namanga eneo lilochukuliwa na Jiji la Arusha.

Wamekubaliana hayo wakati wa mkutano wa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2017/18 na kudai kuwa wakati wa kuanzishwa kwa Jiji la Arusha halmashauri ya Arusha imepata athari kubwa za kuchukuliwa maeneo ya kata za Moshono, Mtevesi n Muriet kwa mqkubalino y kupewa eneo la mita mia 200 ambalo mpaka sasa jiji hilo halijatoa eneo hilo.

Hata hivyo madiwani ho wameilalamikia Halmashauri ya Jiji la Arusha kuwa wagumu katika kutekeleza makubaliano hayo jambo ambalo limeiathiri halmashauri ya Arusha kimapato pamoja na muingiliano wa baadhi ya wakazi kutokujua wanaishi wapi kutokana na kutokuwa na mpaja rasmi kati ya halmashauri hizo mbili.

Madiwani wengi wameonesha kukerwa na suala hilo kwa kuwa wameshazunguka sana kudai eneo hilo bila mafanikio licha ya wakuu wa mikoa kuahidi kumaliza mgogoro huo bila kuzaa matunda.

Hata hivyo wajumbe hao walienda mbali zaidi na kushauri kuwa Halmashauri ya Arusha ifungue mashauri mahakamani kwa ajili ya kudai maeneo yake yaliyochukuliwa na jiji la Arusha endapo njia ya mzungumzo itashindwa kufikia muafaka.

Baraza hilo la kwawaida limejadidi jumla ya agenda 12 ambazo zimelenga kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya halmashauri ya Arusha kwa ajili ya wananchiya maendeleo ya wananchi wake.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo