Tuesday, July 25, 2017

Don Consult Ltd watafiti vyanzo asili vya maji halmashauri ya Arusha

Na Elinipa Lupembe Timu ya watalamu wa halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wataalam washauri wa kampuni ya Don Consult Ltd wamefanikiwa kutembelea na kukagua vyanzo asili vya maji kwa ajili ya kufanya uchambuzi yakinifu 'visibility study' ya mradi mkubwa wa maji utakaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja katika kata nne za na vijiji na vitongoji vitano halmashauri ya Arusha. Watalamu hao wametembelea jumla ya vyanzo sita vya maji ikiwemo chanzo cha Ngaramtoni Well, Mideu na Sambasha, vyanzo vya Tiasilele, Nadung'olo na chanzo kipya kwenye Msitu wa Meru - USA. Mhandisi wa kampuni ya Don Comsult Ltd mhandisi Charles Werema amesema kuwa lengo la kutembele vyanzo hivyo ni kukagua na kupima ubora na kiwango cha maji pamoja na kuangalia ubora wa miundo mbinu ya maji iliyopo kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa mradi huo mpya wa maji. Aidha mhandisi Werema amefafanua kuwa uchambuzi huo yakinifu licha ya kutafiti ubora na kiasi cha maji pia unaangalia uwezo wa vyanzo hivyo vya maji kama unaweza kutosheleza mahitaji ya maji kwenye vijiji na vitongoji vinavyotegemea kuhudumiwa na mradi huo. "Ili kuwa na mradi endelevu tunatakiwa kutafuta vyanzo ambavyo ni sustainabile na vyenye maji ya kutosha" amesisitiza Werema Mhandisi Werema pia amesema kuwa vyanzo asili vinatabia ya kupungua maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi tofauti na vyanzo vya kuchimba ambavyo uwezekano wa maji kwisha ni mdogo sana licha ya gharama kubwa za uendeshaji na matengenezo. Naya mhandisi wa maji halmashauri ya mhandisi Joyce Bahati ameonyesha kuridhishwa na upatikanaji wa chanzo kipya katika msitu wa MERU-USA ambacho hakijawahi kutumika na wingi wa maji unaonekana hata kwa macho. "Tunasubiri matokeo ya uchunguzi utakaofanywa mtaalamu mshauri wa Don- Consultant baada ya kupima maji hayo kwa kuangalia zaidi quality na quantity ya maji ili mradi uanze" amesema Bahati. Hata hivyo mhandisi Bahati amesema wanategemea mradi huo kuwa endelevu kutokana na kuwekwa utaratibu wa kulipia maji kabla ya kutumia kwa kutumia mfumo wa kielekroniki unaojulikana kama ' eWater pay' jambo ambalo utaratibu huu utauwezesha mradi huu kujiendesha na kudumu kwa muda mrefu. Mradi huo wa maji umefadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika la maendeleo DFID unaotegemea kutekelezwa na shirika la WaterAid kwa kushirikiana na halmashauri ya Arudha katika vijiji vya Olkokola na Lengijave pamoja na vitongoji vya Ngaramtoni, Seuri na Ekenywa kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni mradi utakaogharimu shilingi bilion 4.5 na mradi huo utatekelezwa kuanzia mwezi Julai 2017 mpaka Mei 2018.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo