Saturday, August 12, 2017

Karia ashinda Urais TFF azungumza baada ya kuapishwa


Wallace Karia ameshinda kwa kishindo nafasi ya Rais kufuatia uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliofanyika tarehe 12.08,2017 katika Ukumbi wa St Gasper Mjini Dodoma kwa kupata kura 95 kati ya kura halali 125 zilizohesabiwa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya TFF wakili Revocatus Kuuli ametangaza amemtangaza ndugu Wallace Karia kuwa mshindi  nafasi ya urais kwa kupata jumla ya kura 95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa huku kura tatu zikiharibika na Michael Wambura akichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo.

Aidha wakili Kuuli ametangaza matokeo ya wagombea wengine wa Urais pamoja na kura walizopata ni Ally Mayay Tembele (9), Shija Richard (9), Iman Madega (8), Frederick Mwakalebela (3) na Emmanuel Kimbe (1).

Mohamed Abeid (Dodoma na Singida), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Sarah Chao (Arusha na Manyara), Dustan Ditopile (Lindi na Mtwara), Elias Mwanjala (Mbeya na Iringa), Francis (Pwani na Morogoro), Vedastus Lufano (Mara na Mwanza), Lameck Nyangaya (Dar es salaam), Kenneth Pesambili (Rukwa na Katavi), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga), Issa Mrisho (Kigoma na Tabora) na James Patrick (Njombe).

Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa wameapishwa mjini Dodoma muda mfupi baada ya matokeo ya ushindi wao katika uchaguzi huo kutangazwa.

Akitoa hotuba yake muda mfupi baada ya kuapishwa kwake, Rais wa Shirikisho hilo (Wallace Karia) amesema kuwa amepigiwa simu na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na wote wamelipongeza Shirikisho hilo kwa uamuzi ulioufanya na kuutakia uongozi mpya mafanikio mema.

Rai Karia ametaja mikakati yake ya kuiongoza TFF ni pamoja na uwajibikaji, ukweli, uwazi na kufanyakazi kama timu jambo ambalo anaamini litaipeleka soka la Tanzania katika haua nzuri.

Aidha Karia amesema TFF itawapa waandishi wa habari elimu ili kujua mambo gani ya kuzingatia kuweza kuinua soka la Tanzania, huku akitangaza kuwa soka la Tanzania halitakuwa na ubabaishaji.

Naye Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameiagiza TFF kuweka utaratibu wa kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wajue.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo