Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa ALAT umeanza jijini Dar es Salaam huku mwenyeji wa mkutano huo akiwa ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
amesema kupitia mkutano huo wataiomba serikali ili iweze kurudisha vyanzo vya mapato vilivyokuwa katika halmashauri.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu na kuwakaribisha wajumbe wa mkutano huo Meya Mwita amesema licha ya agenda za mkutano huo watawasilisha ombi rasmi kwa serikali la kuiomba kurudishiwaa vyanzo vya mapato vilivyokuwa vikisimamiwa na halmashauri .
Meya Mwita ameeleza kuwa vyanzo vya mapato ambavyo vilikuwa vikisimamiwa na halmashauri vilisaidia kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hususani zile za huduma za kijamii.
Amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni matangazo ya barabarani sambamba na kodi za majego ambapo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zikiiletea halmashauri fedha ambazo zilitumika kuboresha huduma za afya, elimu na barabara.
Aliongeza kuwa kwakuzingatia ustawi wa halmashauri hizo ,mkutano huo utajadili na kumfikishia Rais Dk. John Magufuli ili fedha hizo zirudi kwa ajili ya maendeleo hususani Vijijini, Kata na Majiji.
“ Hali ya Halmashauri nyingi kifedha sio nzuri, na hii ni baada ya vyanzo hivi vya mapato ambavyo tulikuwa tunategemea kuchukuliwa, katika hali yoyote hakuna halmashauri ambayo itakuwa na fedha” amesema Meya Miwta.
Meya Mwita alitolea mfano halmashauri ya Ilala iliyopo katika jiji la Dar es Salaam kuwa kupitia vyanzo hivyo ilikuwa ikikusanya zaidi ya bilioni 68 ambazo zilikuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma za kijamii ndani ya halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Mkutano wa ALAT Gullam Hafidhi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Shinyanga amesema kuwa mkutano huo wa siku tano utafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
No comments:
Write comments