Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta na kubadilishana uzoefu na baadae kufanya ziara Ziwa Eyasi mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ameongoza kikao hicho kilicho washirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema maandalizi hayo ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017.
No comments:
Write comments