Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Arusha inawashikilia zaidi ya watu mia mbili kwa kutokudai risiti mara baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali huku wakifahamu ni lazima kuchukua risiti mara baada ya kununua.
Watu hao wameshikiliwa wakati msako ulioendeshwa na TRA na kuwabaini wanunuzi ambao hawadai risiti pindi wanapofanya manunuzi au kupata huduma pamoja na wafanyabisahara ambao hawatoi risiti hizo ambapo zaidi ya watu mia mbili wamekamatwa.
Meneja msaizi wa Oparesheni hiyo Alex Katundu, amethibitisha kukamwatwa kwa watu hao pamoja na bidhaa mbalimbali ambazo wanunuzi hawakuwa na risiti.
Katundu amesema kuwa watu hao watachukuliwa hatua kwa mijibu wa sheria kwa kuwa kutodai risiti ni kosa kisheria na pia ni kuikosesha serikali mapato.
Baadhi ya wananchi waliokamatwa wamekiri kutodai risiti wakati walipofanya manunuzi.
Kwa mujibu wa TRA muuzaji akishindwa kutoa risiti faini yake ni kuanzia milioni 3, hadi 4, huku mnunuzi akishindwa kupokea risiti faini yake ni kuanzia shilingi Elfu thelathini
Hata hivyo Katundu ameendelea kuwasisitiza wananchi kudai risiti pindi wanapofanya manunuzi pamoja na wafanyabiashara kutoa risiti ili kuepuka kuingia kwenye mgogoro ya kisheria ambao utakulazimu kulipa faini ambayo ni hasara kupoteza fedha kwa uzembe kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu.
No comments:
Write comments