Friday, August 11, 2017

Waziri Lukuvi aagiza aliyekuwa Afisa Ardhi Mteule halmashauri ya Meru kurudishwa kutoka Kibiti

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa Wilium Lukuvi amemwagiza Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ndugu Richard Kwitega kuiandikia barua Wizara ya TAMISEMI kumrejesha aliyekuwa Afisa Ardhi mteule wa Halmashauri ya Meru, ili achukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kuvuliwa wadhifa wake pamoja na utumishi, kutokana na kuuza ardhi ambayo serikali ilishatoa mwongozi wa kuifuta hati yake. Afisa ardhi huyo ni Jeremia Wilson Horoba ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Kibiti na anadaiwa kuuza shamba la Karamu Coffee Estate lenye hekari 244. ambapo inadaiwa aliuza hekari nane. Lukuvi ameongeza kuwa akisharudishwa Arusha avuliwe nyadhifa zote pamoja na kuondolewa katika utumishi kisha hatua nyingine za kisheria zifuate. Mkuu wa mkoa wa Arusha akimkabidhi waziri Lukuvi ripoti ya mapendekezo ya ufutwaji Mashamba makubwa 12 makubwa yaliyopo wilayani Arumeru, amesema mashamba yote yatakayofutwa si yote watapewa wananchi, mengine yatapangiwa utaratibu maalumu Ripoti iliyokabidhiwa ni ya Agizo la Rais Magufuli kwa wakuu wa mikoa yote kuhakiki mashamba yote ambayo hayajaendelezwa yaliyotolewa na serikali. Chanzo PPM MEDIA

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...