Kikosi cha Yanga kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi yake dhidi ya watani wao wa jadi Simba.
Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.
Yanga ilikuwa kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo na msimu mpya wa 2017-18.
Hata hivyo, Yanga wamekuwa wakifanya siri sehemu waliyofikia kwa ajili ya kambi ya mwisho kwa ajili ya mechi hiyo.
No comments:
Write comments