
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali inaendelea na mipango ya utekelezaji wenye lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora kuanzia elimu ya msingi itakayowawezesha mwanafunzi kumudu utumishi wa serikali,sekta binafsi na kujiajiri wenyewe.
Waziri Ndalichako amesema hayo mjini Kasulu wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Grand High School,ambayo ujenzi wake ulikwama kabla ya wizara kutoa Shilingi Blioni 1 za kuendeleza ujenzi huo.
Amesema pamoja na kutoa vifaa vya maabara katika shule zote za sekondari nchini, vyumba vya madarasa 1, 405 vimejengwa katika shule 378.
Kwa upande wao wananchi wameitaka serikali kuipa kipaumbele mikoa ya pembezoni ambayo ipo nyuma kwa kuongeza shule pamoja na vyuo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga ameeleza kuwa zaidi ya shilingi Bilioni 29 zitatumika hadi kukuamilisha ujenzi wa shule hiyo maalum.

No comments:
Write comments