Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC linakusudia kuanza utafiti wa namna ya usambazaji wa miundombinu ya kusafirishia gesi asilia kwenye mikoa mitano ya Dodoma, Mwanza, Tanga, Mbeya na Arusha.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapuuluya Musomba wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea eneo la miundombinu ya gesi asilia na ufuaji umeme kwa kutumia gesi asilia lililopo Kinyerezi jijini Dar es salaam.
Muhandisi Musoba amefafanua kuwa hatua hiyo inakwenda sambamba na kuandaa mpango kabambe wa mtandao wa miundombinj ya Gesi Asilia mkoani Pwani ili kuwezesha viwanda vitakavyojengwa mkoani humo pia vitumie Gesi hiyo Asilia.
Kwa upande wake serikali imebainisha nia yake ya kuhakikisha viwanda vingi nchini vinaunganishwa na matumizi ya gesi asilia ambapo hadi sasa viwanda 37 vimeshaunganishwa .
No comments:
Write comments