Tuesday, August 8, 2017

Simba Day yang'ara yaipiga Rayon Sport 1-0


Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 baada ya kuipiga Rayon Sports katika mechi  ya kuvutia iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba imeibuka na ushindi huo wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa katika tamasha la Simba Day ambalo hufanyika kila mwezi Agosti 8 kusherekea siku maalum ya klabu hiyo.

Bao hilo la pekee la mchezo huo lilifungwa na Mo Ibrahim katika dakika ya 15 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Emmanuel Okwi aliyeingia kwa kasi katika eneo la hatari.


Mashabiki wa Simba wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha la klabu yao la Simba Day.

Ndani ya uwanjani kulishuhudia majukwaa ya mashabiki wa Simba yakiwa yamejaa kufikia saa 8:02 huku mashabiki wakihamia majukwaa ambayo hukaliwa na mashabiki wa Simba.

"Usajili uliofanywa na viongozi unatupa imani kubwa ya kufanya vizuri. Natka kushudia wachezaji wapya kwakuwa nimekuwa nikiwasikia tu kwenye magazeti,"alisema  Kudra Musa.


Mwananchi:

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...