Waumini wa Kanisa Evangelistic Assembly of God lililopo Temeke jijini Dar es salaam wamemuomba rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kuingilia kati mgogoro wa kiwanja baina ya kanisa hilo na Kampuni binafsi.
Waumini hao wamemuomba Rais Magufuli kuingila kati mgogoro huo wa muda mrefu wakiamini anaweza kuleta ufumbuzi dhidi yao na Kampuni hiyo.
Kanisa hilo lenye waumini zaidi ya 1,500 limeingia kwenye mgogoro na kampuni ya Swale Traders limited wa kugombania kiwanja namba 141 kitalu D kilichopo mtaa wa Evereth Manispaa ya Temeke.
Kanisa hilo limedai limepatiwa notisi ya kutakiwa kuondoka kwenye kiwanja hicho ifikapo kesho jumatatu.
Kwa mujibu wa Kanisa la Evangelistic Assembly of God lililopo Temeke jijini Dar es salaam Mgogoro huo umedumu kwa muda wa miaka 39 sasa.
No comments:
Write comments