Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Nchini Gilliard Ngewe amesema haya Mkoani Mbeya wakati wa kikao cha pamoja kati ya wadau wa usafirishaji na Sumatra, ambacho kimelenga zaidi kutoa elimu kuhusu kanuni mpya ambazo zitaanza kutumika January 15 mwaka huu, ikiwemo kanuni mpya ya usafirishaji magari ya abiria ya mwaka 2017 ambayo imeongeza baadhi ya vigezo vya usafirishaji kulingana na teknolojia inavyokuwa.
Amesema baadhi ya magari yanayofanya safari zake kutoka mikoa ya kanda ya ziwa yameshafunga mfumo huo, ambao utawezesha mwenendo mzima wa gari kwa kubaini spidi hata nyakati za usiku, lakini pia mfumo huo utasaidia kuonesha kama kuna madhara yametokea kwa kubonyeza batani maalumu ndani ya gari, lakini pia mfumo huo unadaiwa kudhibiti matumizi mabaya ya mafuta na kutoa faida zaidi kwa mmiliki .
Na Muungwana Blog
No comments:
Write comments