Friday, January 5, 2018

Serikali kuboresha miundombinu ya barabara



 Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Ujenzi imejipanga mikakati ya kuendelea kuboresha miundo mbinu ya barabara zinazounganisha wilaya mikoa na nchi za jirani ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi unaotegemea kilimo na viwanda.

Mkakati huo umethibitishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Elias Kuandikwa wakati akizungumza na wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara nchini ambapo amesema kuwa mkakati huo una lengo la kuchochea uchumi wa kilimo na viwanda nchini Tanzania.


"Ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi ni lazima kuboresha mtandao wa barabara ambao ndio nyenzo muhimu ya kusafirisha malighafi kutoka shambani na bidhaa za viwanda kwenda kwa walaji" amesema Mhandisi Kuandikwa.

Naye kaimu meneja wa bodi ya mfuko wa barabara nchini Rashidi Kalimbaga amesema mtandao wa barabara umeboreka ambapo barabara kuu na za mikoa zenye hali nzuri zimeongezeka kutoka asilimia 79 kwa mwaka 2006/07 hadi kufikia asilimia 87 kwa mwaka 2016/17 na barabara za wilayani kutoka asilimia 55 hadi 57 kwa kipindi hicho.

Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliongea na Redio One wameponge za mafanikio ya serikali katika ujenzi wa barabara hasa zinazounganisha mikoa na mikoa na kuomba mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua watu wanaohujumu miundombinu hiyo ikiwemo kuzidisha uzito wa magari ya mizigo na kuiba alama za barabarani.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo