Friday, December 22, 2017

Pengo la walimu wa vyeti feki lazibwa


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ametangaza ajira mpya 3,033 za walimu wa shule sekondari na msingi nchini watakwenda kujaza nafasi zilizoachwa wazi na walimu waliobainika kuwa na vyeti feki.

Jafo alisema kuwa majina ya walimu hao wapya 3,033 yatatangazwa leo na kupangiwa vituo vya kazi, walimu 266 watakuwa ni walimu wa shule za sekondari na Walimu 2,767 watakuwa walimu wa shule ya msingi.

Aidha Jafo amewataka walimu hao wapya ambao wamechaguliwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa halmshauri husika ambazo watakuwa wamepangia kuanzia Disemba 27, 2018 hadi Januari 7, 2018.

Mbali na hilo Selemani Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambazio walimu hao wataripoti kuwapokea na kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo