Florah Zelothe wa Chama Cha Mapinduzi CCM ameshinda nafasi ya Udiwani kata ya Musa baada ya kuwashinda wapinzani wake kutoka vyama vya ACT -Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika Uchaguzi Mdogo wa kata hiyo uliofanyika leo 26.11.2016.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Musa Twati Sukurieti amesema kuwa Piniel Kinisa wa chama cha ACT-Wazalendo amepata kura 12, Flora Zelote wa CCM amepata kura 2,629 na Eliud Laizer wa CHADEMA amepata kura 1,152.
Sukuriet ametaja idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 5,631 watu waliopiga kura ni 3,892, kura halali ni 3802 na kura zilizokataliwa 90.
Aidha amesema kuwa Flora Zerothe amepata ushindi wa kura 2,629 kati ya kura kura halali 3802 sawa na aslimia 69.14.
Uchaguzi huo wa marudio umefanyika baada ya Mahakama kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba, 2015 ambao Eliud Laizer alishinda mafasi hiyo na baadaye Mahakama kutengua matokeo hayo.
PICHA ZA WANANCHI WALIOJITOKEZA KWENYE ZOEZO LA KUPIGA KURA.
No comments:
Write comments