Serikali ya Tanzania na Japan leo zimesaini makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 1.4 kwaajli ya usanifu wa kina wa mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya New bagamoyo Road, safari hii ukihusu, Makutano ya barabara inayotoka Moroco, Kawawa – Mwenge na kuifanya kuwa ya njia nne.
Usanifu huo ukikamilika,utaruhusu kufanyika kwa upanuzi wa awamu ya pili ya New bagamoyo Road,kufuatia kukamilika kwa kilometa 12.9 za awamu ya kwanza ya Mwenge – Tegeta, ukigharimu shilingi bilioni 99.5 miaka mitatu iliyopita na kusaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero ya msongamano wa magari katika barabara hiyo.
Waziri wa Fedha na mipango Dokta PHILIP MPANGO, akizungumza baada ya kusaini makubaliano ya msaada huo uliotolewa na Japan kupitia shirika lake la maendeleo la JAICA, mbali na kuishukuru nchi hiyo, ameahidi fedha hizo kusimamiwa na kutumika inavyopaswa.
Katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa wakala wa barabara Tanzania(TANROADS),Mhandisi PATRICK MFUGALE, ambao ni wadau wakubwa wa mradi huo amesema, hakuna tena vikwazo vya kukwamisha upanuzi huo.
Balozi wa Japan nchini, MASAHARU YOSHIDA na Mwakilishi mwandamizi wa JAICA nchini, SATORU MATSUYAMA, wameelezea matarajio chanya ya mradi huo na kusisitiza usanifu huo ufanuywe kwa kasi na viwangi stahiki.
No comments:
Write comments