Friday, September 1, 2017

Simba yaomba radhi mashabiki wake


Klabu ya Simba imewaomba radhi mashabiki wa kandanda nchini kwa kuhairisha mechi yao kirafiki iliyopangwa kupigwa leo jioni dhidi ya Hard Rock ya Visiwani Pemba katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

Hayo yameweka wazi kupitia taarifa iliyotolewa na uongozi huo na kusema mchezo kwa sasa utachezwa siku ya Jumapili ya Septemba 3 mwaka huu.

Mchezo huo umesogezwa mbele ili kuweza kuwapisha Botswana ambao kesho watautumia uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Taifa Stars katika mchezo wao kirafiki siku ya Jumamosi Septemba 2.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo