Saturday, September 23, 2017

Rais Magufuli awatunukia Kamisheni maofisa 422 wa JWTZ


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo mbali mbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.

Tukio hilo ambalo limefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbali mabali wa kitaifa, mafisa wa Jeshi nchini pamoja na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani.

Kabla ya kuwatunuku kamisheni maafisa hao wa jeshi, Rais Magufuli alikagua gwaride maalum na kutoa zawadi kwa maafisa wa jeshi watano waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.

Tukio hilo la Rais Magufuli kuwapa Kamisheni Maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni la kwanza kufanyika katika uwanja wa wazi badala ya viwanja vya jeshi wilayani Monduli.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo