Watoto 2 Ikram na Maureen, kati 4 waliotekwa wamepatikana wakiwa wamefariki dunia katika shimo la choo ambacho bado halijaanza kutumika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian huko Olasiti jijini Arusha, Daudi Safari, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi limeopoa miili ya watoto hao leo jioni.
Inadaiwa kuwa mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya kuondoka na kuelekea Geita ambapo amekamatwa na kusema walipo watoto hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha taarifa za kukamatwa kwa mtekaji huyo aliyetambuliwa kwa jina la Samson Petro mwenye umri wa miaka 18.
Kamanda Mwabulambo amesema kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo mwenye miaka miwili.
Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha nyumba hiyo ya kulala wageni wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Ombeni Mshana na Elizabeth Ombeni.
No comments:
Write comments