Wednesday, September 6, 2017

Buswita atua rasmi Yanga


Mshambuliaji Pius Buswita.

Sakata la kiungo mshambuliaji Pius Buswita kufungiwa, ni kama vile limemalizika na mchezjai huyo atakuwa na nafasi ya kuichezea Yanga kama alivyotaka.

Awali mchezaji huyo alidai sheteni alimpitia na akajikuta akisaini mikataba miwili katika klabu za Simba na Yanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias Mwanjala amelizungumza hilo leo Jumatano kwa kusema klabu hizo mbili zimezungumza na kuafikiana juu ya mchezji huyo ambapo Yanga ikikamilisha kile walichozungumza, rasmi Buswita atakuwa mchezaji wa Yanga.

Mwanjala amesema kuwa baada ya Simba na Yanga kukubaliana juu ya mchezaji Pius Buswita ili atoke kifungoni, Yanga itatakiwa kuilipa Simba shilingi milioni 10 ambazo Buswita alizichukua aliposaini Simba.

Amesema kuwa muda wowote fedha hizo zikilipwa basi Buswita ataruhusiwa kucheza, jambo ambalo linaonekana kuwa ni dogo kwa Yanga kulitekeleza.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo