Thursday, August 10, 2017

Majengo ya shule ya sekondari Mwandeti yakamiliaka.

Kutokana na sera ya elimu ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano imwezea kutenga kiasi cha shilingi milioni 259 ambazo zimetumika kwenye ujenzi vyumba vinne vya madarasa, bweni, choo chenye matundu kumi pamoja na ukarabati wa maabara tatu za Baiolojia, Fizikia na Kemia katika shule ya sekondari Mwandet iliypo kata ya Mwandeti halmshauri ya Arusha. Fedha za ujenzi huo zimetokana na mradi unaotekelezwa na serikali wa Lipa kutokana na Matokeo ‘Pay for Result’ maarufu kama P4R ambao utekelezaji wake umeanza mwaka wa fedha uliopita wa 2016/2017 katika halmshauri ya Arusha. Ujenzi huo umekamiliaka kwa asilimia 100% na mpaka sasa majengo hayo yameanza kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano ambapo imesaidia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi kusomea. Aidha ukarabati uliofanywa kwenye vyumba vya maabara utasaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo kwenye masomo ya sayansi na kuongeza wigo wa ufaulu wa wanafunzi katika masomo hayo ambatyo ni miongoni mwa masomo ambayo ufaulu wake umekuwa wa kiwango cha chini kulinganisha na masomo ya Sanaa. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya majengo hayo kati ya uongozi wa shule na mkandarasi aliyefanya ujenzi huo yaliyofanyika shuleni hapo, Mkuu wa shule ya sekondari Mwandet John Masawe alisema kuwa ujenzi huo umetokana na fedha za mradi wa P4R ambapo walipokea kiasi cha shilingi milioni 259 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo hayo ambayo yatatumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita. “tunaishukuru serikali kwa kujenga miundo mbinu ya shule hii ambayo itakuwa chachu ya ufaulu wa wananfunzi wetu kutokana na mazingira ya kujisomea kwa vitendo kuboreshwa na hili litadhihirisha dhamira ya serikali ya elimu bure”. amesema Masawe Aidha Mkuu wa shule hiyo amesema kuwa majengo yote yamekamilika na tayari wanafunzi wa kidato cha sita na cha tano waliopokelewa mwaka huu wameanza kuyatumia madarasa na bweni hali ambayo imepunguza msongamano wa wanafunzi uliokuwepo kwa mwaka uliopita. Naye diwani wa kata ya Mwandeti mheshimiwa Boniface Tarakwa amesema kuwa kutokana na juhudi zilizofanywa na serikali uongozi wa kata kwa kushirikiana na wananchi wametoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ambapo itasaidia kupunguza tatizo la walimu kuishi mbali na vituo vya kazi. Amesema kuwa licha ya mipango mikakati ya miundo mbinu ya shule hiyo kukamilika kwa asilimia kubwa lakini bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa huduma ya maji kwa wanafunzi shuleni hapo. “Tumejipanga vizuri kutatua changamoto hiyo kwa kutoa tawi la maji kutoka kwenye kijiji cha Losikito kwenye mradi wa maji wa World Bank ili maji yaweze kutosheleza shuleni hapo” amesema Mhe. Tarakwa. Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Jackline Isack ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita na kiranja mkuu wa shule (Head Girl) amesema kuwa majengo hayo yamewafanya kuishi vizuri wawapo shule kwa upande wa masomo na malazi kwani hapo awali walikuwa wanabanana madarasni n ahata bwenini lakni sasa hakuna usumbufu huo tena. “Kwa sasa tuko vizuri kiakili na kisaikolojia kwani tunaishi mazingira mazuri ambayo na hakika yataongeza ufaulu kweu wanafunzi kutokana na mazingira yanayotuvutia wanafunzi wote” amesema Jackline

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...