Makatibu muhtasi serikalini wametakiwa kufanyakazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutunza siri za nyaraka mbalimbali za serikali katika maeneo yao ya kazi wakati wa mafunzo ya siku tano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa halmshauri ya Arusha wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Afisa Elimu Taaluma Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Arusha ndugu Charles John amefunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mheshimiwa Alexander Mnyeti, amewataka makatibu muhtasi hao kufanyakazi kwa weledi kwa kuwa taaluma yao iko katika kutunza siri za serikali na za watumishi kwa ujumla.
Ameeleza kuwa taaluma yenu inahitaji weledi na hekima ya hali ya juu katika utunzaji wa siri ndio maana katika serikali kuna masijala bayana ambayo ni ya wazi na masijala ya siri ambayo ninyi peke yenu ndio wahusika wa kutunza nyaraka hizo, hivyo ni vyema mkawa na tabia ya kujizuia kutoa siri kabla ya wakati wa kuweka jambo wazi.
“Si vizuri kukuta nyaraka za serikali tena zina muhuri wa siri zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kama ninyi mkiwa weledi katika utunzaji wa nyaraka hizo, hivyo mafunzo haya yakawafanye muanze upya kurejea taaluma zenu katika maeneo yenu ya kazi na kutambua kuwa serikali imewapa dhamana ya kazi hiyo” amesema Chale
Chale ameongeza kuwa ni ngumu sana kutunza siri lakini kutokana na kazi yenu hamna budi kufanya kutunza siri kwani ndio taaluma yenu mliyosomea na kuapa kuitumikia wakati wote muwapo kazini.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Muda Mfupi kutka chuo cha Utumishi wa Umma Tabora ndugu Musa Ligembe amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watumishi hao juu ya utunzaji wa nyaraka za siri za serikalina kuhudumia wateja wakorofi na wasumbufu katika maeneo yao ya kazi.
Ligembe amesema kuwa mafunzo haya pia yanawakumbusha Makatibu Muhtasi namna ya kuwahudumia wasimamizi katika sehemu zao za kazi, wajibu na majukumu yao pamoja na kuonyesha weledi katika kada zao.
Aidha Ligembe amesema kuwa mafunzo haya yanatolewa mara kwa mara kwa ajili ya kuwafanya makatibu muhtasi kutekeleza majukumu yao kwa kuendana na mabadiliko ya mara kwa mara yanaotokana na amendeleo ya sayansi na teknolojia.
Katibu Muhitasi Idara ya Elimu Sekondari halmshauri ya Geita ndugu Salome Enos amesema kuwa licha ya mafunzo hayo kuwa na umuhimu kwao lakini pia yanawawezesha kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili kada yao kulingana na huduma nyeti wanayoitoa katika ofisi.
A
“Mafunzo haya ni mazuri sana ktukana na ukweli kwamba kila mtu anachangamoto katika kutekeeza majukumu ya kila siku, tukikutana hapa tunapeana uzoefu wa namna nzuri na sahihi ya kukabiliana na changamoto zetu” amesisitiza Enos.
Mafunzo hayo ya siku tano yamefungwa leo na yamehusisha makatibu Muhitasi na Makatibu Mahususi kutoka Ofisi za Wakala wa Serikali, Vyuo pamoja na Ofisi za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Thursday, August 10, 2017
Makatibu muhtasi watakiwa kutunza siri za Nyaraka za Serikali
No related post available
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments