Wednesday, July 19, 2017

Watakaotoa na kusambaza siri za serikali mtandaoni jela miaka 20


Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawaka Bora mheshimiwa Angella Kairuki ametoa onyo kali kwa watumishi wa umma wanaotoa na kusambaza siri za serikali kwenye mitandao ya jamii kuchukuliwa hatua za kisheria.

Waziri Kairuki ametoa onyo hiyo kwa watumishi wa umma wakati akifungu mkutano wa watumishi wa umma wa Manispaa mya ya Ubungo.

Mheshimiwa Kairuki amesisitiza kuwa serikali itachukua hatua za kisheria kwa mtumishi wa umma atakayejihusiha na utoji na usambazaji wa taarifa za serikali atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha mika ishirini jela.

"Mtumishi yoyote atakayehusika na usambazaji wa taarifa za serikali kwenye mitandao ya kijamii atafikishwa mahakamani na ikithibitika adhabu yake ni miaka ishirini jela". amesisitiza Waziri Kairuki.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo