Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha wamekubaliana kutoa ushirikiano mkubwa kwa wataalamu wa halmashauri ya Arusha katika kusimamia Miradi kwa kupitia Mfumo Mpya wa Ruzuku ya Serikali ya Miradi ya Maendeleo 'Local Government Development Grant ' (LGDG ).
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Mh. Noah Lembri wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya Mafunzo ya siku moja ya Mfumo Mpya wa ruzuku ya serikali ya Miradi ya Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Arusha.
Mh. Lembris amesisitiza kuwa wajumbe wa baraza la madiwani wako tayari kushirikiana na watumishi wote kwa kusimamia fedha za ruzuku za miradi ya maendeleo kwa kuwa lengo la mfumo huo ni kuhakikisha miradi inasimamiwa vizuri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na halmashauri kwa ujumla.
Mwenyekiti Lembris amewataka wataalamu wote kusimamia fedha za miradi kwa kufanyakazi kwa nidhamu, uadilifu kwa kufuata miongozo, kanuni, sheria na taratibu za matumizi sahihi you a fedha za serikali.
Pia ameutaka uongozi wa halmashauri kuwa wazi katika kutekeleza majukumu pamoja na kutoa taarifa mapema endapo kuna tatizo lolote kuliko kusubiri mpaka mambo yaharibike.
Hata hivyo Mkurugenzi Mendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera ameahidi kusimamia vema mfumo huo na kuwashughulikia watumishi watakaoenda kinyume na taratibu hizo au kuleta uzembe katika utekezaji wa miradi.
Mkutano huo licha ya kujifunza mfumo mpya wa ruzuku ya serikali pia mkurugenzi wa halmashauri Dkt. Mahera aliwasilisha taarifa ya Mpango Mkakati wa halmashauri ya Arusha kwa miaka mitano ambao madiwa hao waliupitisha na kuomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa watendaji wa halmashauri sambamba na kubuni miradi ya kuongeza mapato ndani ya
No comments:
Write comments