Wajumbe wa baraza la mdiwani halmashauri ya Arusha wameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa kuwezesha kupata hati safi kufuatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Pongezi hizo zimetolewa baada ya Mweka Hazina wa halmashauri ndugu Munguabela Kakulima kutoa taarifa hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi Machi, 2017 katika mkutano wa baraza la madiwani.
Mweka Hazina huyo alisema kuwa halmashauri ya Arusha imefanikiwa kupa hati safi kwa mwaka wa fedha 2015/16 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.
"Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kulitaarifu baraza lako tukufu kuwa halmashauri yetu imapata hati safi kwa mara ya tatu mfululizo " alisema Kakulima
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mheshimiwa Noah Lembris ametoa pongezi kwa uingozi wa halmashauri pamoja na wadau wa maendeleo kwa ushirikiano wao uliopelekea kupata hati safi.
"Nitoe pongezi zangu za dhati kwa mkurugenzi, Idara ya Fedha, watumishi wote, wadau wa maendeleo pamoja na wajumbe wa baraza hili la madiwani kwa pamoja wamesababisha upatikanaji wa hati safi " alisema Mwenyekiti
Hata hivyo Mheshimiwa Lembris amewataka watumishi wa halmashauri kufanyakazi kwa uadilifu kwa kusimamia kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya usimamizi na matumizi ya fedha ili halmashauri iendelee kupata hati safi hata kwa mwaka huu tena.
Hata hivyo Mweka Hazina huyo alisema kuwa upatikanaji wa hati safi unategemea zaidi matumizi yanayozingatia kanuni, taratibu na sheria pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wa ndani na nje ya halmashauri hasa wajumbe wa kamati ya ukaguzi.
Halmashauri ya Arusha imepata hati safi kufuatia ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali iiyowasilishwa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali Prof. Mussa Jumma Assad aliyoiwasilisha kwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
No comments:
Write comments