Wednesday, June 21, 2017

Wafanyakazi makao makuu watoa kitita cha fedha kuchangia ujenzi wa madarasa Sokon II



Wafanyakazi wa makao makuu ya halmashauri ya Arusha wameungana na wadau mbalimbali wa maendelea wa halmashuri hiyo kuchangia ujenzi unaoendelea wa vyumba tisa vya madarasa katika shule ya sekondari Sokon II kata ya Sokon II.

Wafanyakazi hao wakiongozwa na Mkurugenzi wao wamechangia kitita cha fedha kiasi cha fedha za kitanzania shilingi 1,000,000/- (milioni moja) kwa ajili ya uwekaji wa vioo kwenye madarasa ya shule ya sekondar ya Sokon II kama ishara ya kuwaunga mkono wadau mbali mbali wa maendelo waliojitokeza kuchangia ujenzi wa madarasa hayo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo kwa niaba ya watumishi wa halmshauri makao makuu waliochanga fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Daktari Wilson Mahera amesema ameshirikiana na watumishi wake kutoa kiasi hicho cha fedha ili fedha hizo zikasaidie kuweka madirisha katika vyumba vya madarasa ya shule hiyo.

“Nimefurahi watumishi kuungana na wadau wengine wa maendeleo kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ingawa sisi ni wasimamizi lakini tumeona ni vema kuungana na wananchi wengine kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika halmshauri yetu” alisema Dk. Mahera
Naye Mchumi wa halmashauri ndugu Nhojo Kushoka anesema ameridhishwa na kitendo cha watumishi kuchangia ujezi wa shule hiyo kwa kuwa kuna wakati watumishi wanatakiwa kuingia mfukoni kwa ajili ya kuwatia moyo wanachi tunaowatumikia.

“Kiuchumi fedha hiyo ni kidogo ukilinganisha na gharama ya mradi lakini kiwango hicho ni kikubwa kiuchumi kina matokeo makubwa kwenye mradi” alisisitiza Kushoka
Diwani wa kata ya Sokon II mheshimiwa Elias Loshula amesema amefurahishwa na kitendo cha watumishi hao kuwaunga mkono jambo ambalo hakulitegemea hivyo alimshukuru mkurugenzi wa halmashauri kwa niaba ya wafanyakazi wote wa makao makuu na kumpongeza mkurugenzi kwa ushirikiano anaoutoa katika usimamizi wa miradi inayotekelezwa kwenye kata yake.

“Ninamshukuru Mkurugenzi Mahera ananipa ushirikiano mkubwa, kila ninapokuja kufuatilia masuala ya kata yangu ya Sokoni II, yuko bega kwa bega na wala hachoki kutembelea miradi inayotekelezwa katika kata yangu, kwa hilo ninampongeza sana” alisema diwani huyo 
Mkuu wa shule ya Sokoni II mwalimu Kilonzo mara baada ya kupokea kitita hichi cha fedha hakusita kutoa shukurani zake za dhati kwa watumishi wa makao makuu kwa kisi cha fedha walichojitoa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madaras Sokoni II

“Unajua kutoa ni moyo hivyo ninashukuru sana kwa kuwa licha ya ugumu wa maisha lakini wamejitoa kwa moyo zaini niajivunia kuna shule nyingi lakini Sokon II imeonekana zaidi hili ni jambo la kujivunia sana kwa kweli.” Alimaliza Mwalimu Kilonzo
Shule ya Sekondari Sokon II inafanya ujenzi wa umaliziaji wa ghorofa ya pili wenye jumla ya vyumba vya madarasa vitano vyenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 225 kwa wastani wa wanafunzi 45 kwa darasa ujenzi ambao umechangiwa na serikali, wadau mbalimbali kwa kushirikiana na wanchi wa kata ya Sokoni II.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo