Wednesday, June 21, 2017

HALMASHAURI YA ARUSHA YAZINDUA BARAZA LA WATOTO LA HALMASHAURI HIYO


Halmashauri ya  Arusha imeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa kuzindua Baraza la watoto la halmashauri la halmashauriya Arusha.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha yaliwakutanisha jumla ya watoto 81 kutoka  katika kata zote 27 za halmashauri ambapo kila kata iliwakilishwa na watoto watatu kutoka katika mabaraza ya watoto ngazi ya kata waliounda Baraza la watoto la halmashauri.


Afisa Maendeleo ya Jamii Neema Mwina amesema lengo la kuunda baraza hili ni kuwa wezesha watoto kutambua haki zao za msingi ili waweze kuzisimamia wenyewe kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. 


Baraza hilo la watoto lilizinduliwa na aliyekuwa mgeni rasmi Diwani Viti Maalumu CCM mheshimiwa Yasmin Bachu kwa niaba ya mkuu wawilaya ya Arumeru kwa kuisisitiza jamii kuhakikisha mtoto anapatiwa haki zake za msingi bila kubaguliwa kwa kuimarisha ulinzi kwa watoto.


Bachu alizitaka  asasi za serikali na zisizo za serikali kusaidia jamii kusimamia utekelezaji wa haki hizo za msingi za watoto kutokana na changamoto nyingi . 

Awali maadhimisho hayo yalitanguliwa na risala iliyosomwa na watoto hao na kufuatiwa uchaguzi wa viongozi wa Baraza hilo la watoto ambao watakuwa wajumbe wawakilishi kwenye Baraza la watoto la mkoawa Arusha.

Mtoto Sumaiya Abdul mwanafunzi wa shule ya msingi Olosiva kata ya Oloirien mwenye umri wa miaka (11) alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza hilo la watoto na katibu wake Catherine Elisantemiaka (9) mwanafunzi w ashule ya msingi Mzumuni kata ya Nduruma.


Hata hivyo mheshimiwa Bachu alitoa zawadi yashilingi 200,000/- kwa ajili ya kufungulia akaunti ya Baraza hilo na kuungwa mkono na Diwani wa kata ya Sambasha mheshimiwa Sabaya na diwani viti maalum mhe,
Muna Talibw a aliotoa kwa  pamoja shilingi 100,000/- na kufanya jumla ya shilingi 300,00/-
Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni "MAENDELEO ENDELEVU 2030 IMARISHA ULINZI NA FURSA SAWA KWA WATOTO "

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo